Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2020

Kisukari (Diabetes)

Utangulizi Unapokula chakula cha wanga kama vile ugali,wali, matoke,mihogo,viazi  n.k hubadilishwa kuwa sukari iitwayo glukozi. Glukozi ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya nishati.Sukari hii hudhibitiwa na homoni iitwayo insulini,inayotolewa na kiungo kinachoitwa kongosho kilichopo katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.   Kisukari ni ugonjwa unaosababisha na mwili kushindwa kubadili glukozi kuwa nishati,hivyo kusababisha kiwango cha sukari kuwa kingi katika mzunguko wa damu.  Kwa lugha ya kitaalamu huitwa Diabetes Mellitus .Kuna aina nyingi za kisukari lakini kwa kurahisisha,kwa leo tutagawanya katika aina kuu tatu. Aina ya kwanza  Pia huitwa inslini tegemezi. Kongosho hushambuliwa na magonjwa ya kingamaradhi(autoimmune) na kushindwa kutoa homoni ya insulini. Kisukari cha aina hii humpata mtu akiwa katika umri mdogo. Dawa yake ni mgonjwa kupatiwa insulini. Aina ya pili Huu ni ugonjwa wa kurithi. Aina hii huwapata zaidi watu wanene na wanene kupindukia. Watu wanene wana kiasi kikubwa c

Homa ya Kichaa cha Mbwa

Utangulizi Kichaa cha mbwa ni nini? Ni ugonjwa hatari unaotokana na maambukizi ya virusi vijulikanavyo kama rabies kwa kiingereza. Maambukizi hayo hutokea baada ya kung'atwa, kukwaruzwa na makucha au kulambwa machoni,puani, mdomoni au katika jeraha na mbwa, paka  au popo aliye na virusi hivyo.  Tofauti na virusi,unapong'atwa na mbwa au paka ni hatari ya kupata maambukizi ya bakteria katika majeraha ambayo husababisha maumivu makali na kuchelewesha kupona kwa majeraha hayo kama hatua hazitachukuliwa haraka. Lakini pia kupata majeraha sehemu za viungo( joints ) kunaweza kumsababishia mgonjwa ulemavu wa kudumu. Nchini Tanzania pekee inasadikiwa kuwa watu 1500 hufariki kila mwaka kutokana na kichaa cha mbwa, ugonjwa unaoweza kuzuiwa kwa asilimia 100 kwa kutumia chanjo(DW). Nini cha kufanya unaposhambuliwa na mbwa, paka au popo?  Kuna hatua muhimu kadhaa za kufanya pindi unaposhambuliwa na mbwa, paka au popo. Safisha majeraha kwa maji yanayotiririka na sabuni bila kusugua kwa dakik

Homa ya Findofindo (Tonsillitis)

Utangulizi   Findofindo ( Tonsillitis) ni nini?  Mafindofindo ni mashambulizi ya virusi au bakteria kwenye tezi za koo zijulikanazo kama findo. Asilimia 15 mpaka 30 ya mashambulizi haya yanatokana na bakteria ila asilimia kubwa hutokana na virusi.  Dalili za mafindofindo   Kwa kawaida ni ngumu kutofautisha kati ya maambukizi yatokanayo na bakteria na yale ya virusi ila leo nitakujuza siri ndogo. Zipo dalili za pamoja na zile za tofauti.  Zifuatazo ni dalili za pamoja za mafindofindo unazoweza kuzipata kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya bakteria na yale virusi  Maumivu ya koo Kupata shida katika kumeza  Homa kali ( Zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)  Maumivu ya kichwa  Maumivu ya sikio  Utando katika findo Dalili zifuatazo zinaasilimia kubwa sana kupatikana kwa mtu mwenye mashambulio yatokanayo na virusi.  Homa ( zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)   Uvimbe shingoni ( upande mmoja au pande mbili)   Maumivu ya kichwa  Kutokwa na kamasi  Kutokwa na machozi   Kumeza kwa shida  Maum

Msongo wa Mawazo (Depression)

Msongo wa mawazo ni nini? Msongo wa mawazo  ( Depression ) ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo hutokana na pale mtu anaposhindwa kukabiliana na jambo linalomtatiza. Msongo wa mawazo huwapata watu wa rika na asili zote. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake  hupata msongo wa  mawazo zaidi kuliko wanaume. Msongo wa mawazo ni tatizo la kimwili pamoja na kiakili. Dalili. kujisikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa, kukosa hamu ya kula au kula chakula kupitiliza,hasa vyakula vyenye madhara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuwa na huzuni wakati wote na kujisikia mnyonge, kusahau kirahisi au kupungua kwa uwezo wa kufikiria, kujisikia mpweke au kukosa matumaini ya maisha, kupungua kwa uwezo wa kimasomo kwa wanafunzi, kuwa na hofu au kutokujiamini, kupungua au kuongezeka uzito bila kupenda, kushindwa kulala au kulala kupindukia, kukosa utulivu wa nafsi, kuba

Shinikizo la damu (Hypertension)

Utangulizi Unaweza kuwa na shinikizo la damu (presha) kwa muda mrefu bila kuwa na dalili zozote. Muda wote huu ingawa unakuwa hauna dalili, uwepo wa shinikizo la damu huendelea kuathiri mishipa ya damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama vile magonjwa ya moyo na kiharusi.   Hivyo ni vizuri kujipima mara kwa mara ili kuepuka kuchelewa.     Shinikizo la damu hutokea taratibu kwa kadri umri unavyozidi kuongezeka, hivyo kuathiri karibu kila mtu anapofikia umri mkubwa. Upimaji wake ni rahisi kwa hiyo ni vema ukapima ili kuweza kupambana na ugonjwa huu kwa msaada wa daktari. Dalili Watu wengi wana shinikizo la damu bila kujua au kuwa na dalili. Ni wachahe wanaweza kuwa na dalili kama vile kuumwa kichwa,kutokwa na damu puani na kupata shida ya kupumua. Dalili hizi si maalumu ( spesific) na mara nyingi hazitokei mpaka shinikizo linapokuwa katika kiwango kinachohatarisha maisha. Shinikizo la damu hutokea kwa namna mbili; Kwanza:  Hutokea bila uwepo wa ugonjwa sab

Virusi Vya Korona

Virusi vya Korona ni nini? Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.  Mwishoni mwa Mwaka 2019,huko nchini China katika mji wa Wuhan kulitokea mlipuko wa  virusi vya korona vilivyopewa jina la COVID-19( Corona virus disease 2019) Baada ya muda mfupi mlipuko huo ulienea sehemu mbalimbali Duniani,hasa katika nchi za Korea ya Kusini, Italya, Iran na Nchi mbalimbali za Ulaya.  Kulingana na maambukizo kusambaa haraka, Shirika la Afya duniani lilitangaza mlipuko huu kuwa wa ngazi ya Pandemia tarehe 30 Januari 2020. Hadi sasa ugonjwa huu umeenea kote Duniani na kusababisha maambukizi kwa zaidi ya   watu 2,320 ,000  vifo zaidi ya watu 160,000 ; huku nchi ya Marekani ikiwa inaongoza kwa idadi   ya wagonjwa wanaozidi laki saba. Ugonjwa wa korona unaambukizwaje? Ugonjwa wa korona unaambukizwa kwa virusi vinavyoachwa hewani kwa