Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2021

Mshtuko wa Moyo (Heart Attack)

  Utangulizi Mshtuko wa Moyo hutokea wakati mshipa au mishipa ya damu inayoenda kwenye misuli ya moyo inapoziba na kushindwa kuipatia oksijeni misuli hiyo. Mishipa hiyo huziba kutokana na kuongezeka kwa mafuta aina ya kolesterol kwenye kuta za mishipa hiyo iitwayo  coronary arteries. Mshtuko wa moyo ni tatizo la dharura ambalo lisiposhughulikiwa kwa haraka husababisha kifo. Dalili Kupata maumivu makali ya kifua, mikono hasa wa kushoto,shingoni, mgongoni au kwenye taya ghafla na kuhisi kama kugandamizwa na kitu kizito kifuani, Kuhisi kichefu chefu,maumivu ya tumbo, Kutokwa na jasho la baridi, Kupatwa na kizunguzungu, Kuhisi uchovu wa ghafla, Kushindwa kupumua. Sio kila mtu hupatwa na dalili hizi. Wengine husikia maumivu kidogo huku wengine dalili ya kwanza ni moyo kusimama.Lakini mara nyingi mtu akipatwa na dalili kadhaa kati ya hizo hapo juu kuna uwezekano mkubwa kuwa amepatwa na mshtuko wa moyo. Sababu Kama nilivyosema kwenye utangulizi,mshtuko wa moyo hutokea baada ya misuli ya moyo