Fistula ni nini? Fistula ni tundu lisilo la kawaida ambalo hutokana na kuungana kwa sehemu ya chini ya utumbo mpana (njia ya haja kubwa) na njia ya mkojo au njia ya uke, hivyo kumfanya mgonjwa kushindwa kuzuia haja au kutokwa na hajak ubwa ukeni. Mara nyingi husababishwa na kujeruhiwa kwa sehemu hizo wakati wa kujifungua hasa kwa wanawake wanaozaa katika umri mdogo au wanaokosa msaada stahiki wakati wa kuzaa. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, inakadiriwa kuwa wanawake zaidi ya milioni mbili kutoka Afrika na Asia wanaishi na ugonjwa huu, bila kupatiwa matibabu yoyote, kwa upande wa Tanzania wengi wamekua wakitafuta msaada kwa waganga wa jadi. Nini Husababisha Fistula? Ugonjwa wa Fistula unaweza kusababishwa na mambo kadhaa ikiwemo yafuatayo; Majeraha wakati wa kujifungua, Maambukizi ya Mfumo wa uzazi (PID), Mgonjwa ya utumbo mpana kama vile Crohn , Saratani ya mfumo wa uzazi au utumbo mpana, Majeraha yanayotokana na ajali au upasuaji wa sehemu ya nyonga. Fistula husababisha m
Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia) ni nini? Ni ukuaji wa tezi dume ambalo lipo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume hivyo kusababisha matatizo mengi hasa ya kibofu, figo na njia ya mkojo kwa ujumla. Hii hutokana na kuzibwa kwa njia ya mkojo kitu ambacho huleta madhara kwenye viungo husika. Tatizo hili huzidi kadri umri unavyoongezeka. Kwa kawaida ukubwa wa tezi ni sawa na kipira cha golf , lakini linaweza kukua hadi kufikia ukubwa wa chungwa hivyo kusababisha matatizo. Tezi dume kazi yake ni kutoa majimaji ya shahawa ( semen ) yanayosaidia kulinda, kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume ( sperms ) ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke. Karibu nusu ya wanaume wenye umri kati ya miaka 51 mpaka 60 na zaidi ya asilimia 90 ya wenye umri wa miaka 80 na zaidi wana tatizo hili. Ukuaji wa tezi dume sio saratani lakini wakati mwingine vyote viwili humpata mtu mmoja. Dalili Kujisikia kukojoa muda wote au kushindwa kubana mjoko, Kukojoa kila mara hasa wakati wa usiku, Kuwa na s