Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2022

Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia- BPH)

Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia) ni nini? Ni ukuaji wa tezi dume ambalo lipo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume hivyo kusababisha matatizo mengi hasa ya kibofu, figo na  njia ya mkojo kwa ujumla. Hii hutokana na kuzibwa kwa njia ya mkojo kitu ambacho huleta madhara kwenye viungo husika. Tatizo hili huzidi  kadri umri  unavyoongezeka. Kwa kawaida ukubwa wa tezi ni sawa na kipira cha golf , lakini linaweza kukua hadi kufikia ukubwa wa chungwa hivyo kusababisha matatizo. Tezi dume kazi yake ni kutoa majimaji ya shahawa ( semen ) yanayosaidia kulinda, kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume  ( sperms ) ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke. Karibu nusu ya wanaume wenye umri kati ya miaka 51 mpaka 60 na zaidi ya asilimia 90 ya wenye umri wa miaka 80 na zaidi wana tatizo hili. Ukuaji wa tezi dume sio saratani lakini wakati mwingine vyote viwili  humpata mtu mmoja. Dalili Kujisikia kukojoa muda wote au kushindwa kubana mjoko, Kukojoa kila mara hasa wakati wa usiku, Kuwa na s

Homa ya Mfumo wa Uzazi (Pelvic Inflamatory Disease- PID )

Homa ya Mfuko wa Uzazi ni nini? Ni magonjwa yanayompata mwanamke katika uke, shingo ya uzazi,mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi na sehemu inayozunguka mfumo wa uzazi. Karibu asilimia 85 ya watu wanaopata homa hii hutokana na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, wengi wao wakiwa na vimelea vya bakteria kama vile  kisonono (gonorrhoea) , kaswende (syphilis) , klamidya n.k. Wakati mwingine mgonjwa hupata homa hii kutokana na bakteria ambao kawaida huwa wapo mwilini na hawana madhara lakini kwa sababu mbalimbali kama kupungua kwa kinga, kisukari, saratani, upasuaji, kuwa na magonjwa ya mfumo wa chakula n.k wanasababisha homa.   Dalili Maumivu makali chini ya kitovu na kiunoni, Maumivu wakati wa tendo la ndoa, Maumivu wakati wa kukojoa, Maumivu makali au kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, Kutokwa na majimaji yenye harufu kali  na rangi ya njano, kijani au kahawia ukeni, Kuwa na homa jotoridi 38.3 au zaidi, Kujisikia uchovu, kichefuchefu n.k.   Sababu Homa ya mfumo wa uzazi mar

Saratani ya Matiti (Breast Cancer)

Utangulizi Saratani ya Matiti ni nini? Ni aina ya saratani inayoathiri matiti au maziwa kwa mwanamke au nadra pia kwa mwanaume. Hii hutokana na chembehai( cells) za sehemu yoyote ya ziwa au yote mawili kukua kuliko kawaida na kusababisha uvimbe, maumivu, kutokwa na majimaji,damu au usaha kwenye matiti. Wakati mwingine aina hii ya saratani inaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye kwapa, misuli ya kifua, mishipa ya damu, shingoni n.k.  Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2020, wanawake milioni 2.3 waligunduliwa kuwa na saratani ya matiti, takriban laki saba walifariki kwa saratani ya matiti. Kutoka mwaka 2015 hadi 2020 wanawake milioni 7.8 waligunduliwa kuwa na maradhi hayo, kuifanya saratani ya matiti kuwa ya kwanza kwa kuenea duniani. Ni muhimu kutambua kwamba sio kila uvimbe uliopo kwenye maziwa ni saratani, hivyo ni vyema kumuona Daktari unapokuwa na dalili yoyote nitakayotaja hapo chini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.  Nini husababisha saratani ya mat

Ualbino (Albinism)

 Ualbino ni nini? Ualbino ( albinism ) ni hali ya kiafya inayotokana na mwili kukosa uwezo wa kutoa homoni aina ya melanin . Homoni hii pamoja na kazi nyingine inahusika na utoaji wa rangi ya mwili. Ukosefu wa melanin huathiri ngozi, macho na nywele.  Ualbino ni hali ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ikumbukwe kuwa  Albino sio mgonjwa bali ni mlemavu wa macho, nywele na ngozi ambavyo huathiri maisha yake ya kila siku, hata kufupisha umri wa kuishi. Nje na binadamu ualbino unaathiri pia wanyama, samaki, wadudu, nyoka, mijusi, ndege na hata mimea (kwa mimea hutokana na ukosefu wa klorofili).  Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua kupendelea kuitwa "watu wenye ualbino" kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo au mizimu. Kuenea kwa Ualbino Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya 20,000 duniani ni albino, lakini kwa sababu zisizofahamika barani Afri

Kifua Kikuu (Tuberculosis)

  Utangulizi Kifua kikuu ni ugonjwa hatari sana unaosababishwa na vimelea vya  bakteria vinavyoitwa    Mycobacterium tuberculosis  (MBT),  wanaoshambulia  sehemu mbalimbali za mwili hasa mapafu. Asilimia kubwa ya watu wenye kifua kikuu hawana dalili za kuugua ( latent ). Karibu asilimia 10 ya watu hawa hupata dalili baadae ( active ) na hatimaye nusu yake hufariki  kwa ugonjwa huo. Vimelea vya Kifua Kikuu huambukizwa kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa (kupumua). Utafiti uliofanyika mwaka 2018 ulionyesha kuwa robo ya watu wote duniani wana vimelea vya Kifua Kikuu. Mwaka 2020 watu karibu milioni 10 walipata Kifua Kikuu chenye dalili (active) , watu milioni moja na nusu walifariki kwa Kifua Kikuu, kuufanya ugonjwa huu kuwa wa pili kwa  kuua watu wengi duniani kwa magonjwa ya kuambukizwa ukiongozwa na COVID-19. Nchi nane zinazoongoza kwa wangonjwa wa TBC ni  India (27%), China (9%), Indonesia (8%), the Ufilipino (6%), Pakistan (6%), Nigeria (4%), na Bangladesh (4%). Dali

Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

Ni vidonda vinavyotokea kwenye ukuta wa ndani wa tumbo au utumbo mwembamba.  Hutokana na tindikali( stomach acids ) zinazotolewa na tumbo kusaidia mmeng'enyo wa chakula kuzidi hivyo kuharibu ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba.  Watu wengi wanaweza kuwa vidonda vya tumbo bila kuwa na dalili zozote. Lakini wakati mwingine vidonda vinaweza kutoka damu hadi kuhatarisha maisha kama hatua za dharura hazitachukuliwa. Sababu Sababu kubwa ya vidonda vya tumbo ni maambukizi ya bakteria anayefahamika kwa jina  la Helicobacter pylori(H. pylori).  Matumizi ya dawa za maumivu kama vile ibuprofen(advil,ibucold, motrin IB n.k), aspirin, na naproxen  kwa muda mrefu. Pombe na sigara. Msongo wa mawazo na matumizi ya viungo vya chakula havisababishi vidonda vya tumbo lakini vinazidisha dalili za maumivu kwa mtu ambaye tayari ana vidonda. Dalili Maumivu ya tumbo sehemu iliyopo  kati ya kitovu na kifua, hasa wakati wa njaa kama vile usiku au kati ya mlo mmoja hadi mwingine. Maumivu hupungua baada ya kul