Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Virusi Vya Korona


Virusi vya Korona ni nini?

Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya
kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV. 



Mwishoni mwa Mwaka 2019,huko nchini China katika mji wa Wuhan kulitokea mlipuko wa
 virusi vya korona vilivyopewa jina la COVID-19( Corona virus disease 2019)

Baada ya muda mfupi mlipuko huo ulienea sehemu mbalimbali Duniani,hasa katika nchi za
Korea ya Kusini, Italya, Iran na Nchi mbalimbali za Ulaya. 

Kulingana na maambukizo kusambaa haraka, Shirika la Afya duniani lilitangaza mlipuko
huu kuwa wa ngazi ya Pandemia tarehe 30 Januari 2020.
Hadi sasa ugonjwa huu umeenea kote Duniani na kusababisha maambukizi kwa zaidi ya watu 2,320,000  vifo zaidi ya watu 160,000; huku nchi ya Marekani ikiwa inaongoza kwa idadi ya wagonjwa wanaozidi laki saba.

Ugonjwa wa korona unaambukizwaje?

Ugonjwa wa korona unaambukizwa kwa virusi vinavyoachwa hewani kwa kupiga chafya au kukohoa na kwa njia ya mgusano baina ya watu pale panapokuwa na mgonjwa.
Ukimgusa mtu halafu ukagusa macho,pua, mdomo au kula chakula bila kunawa mikono. 

Kumbuka sio kila mtu mwenye korona anakuwa na dalili,hivyo hasa watu wasio na dalili
ndio wana uwezekano mkubwa wa kusambaza virusi. 

Dalili.

Dalili zake ni pamoja na;
  • Homa,
  • Kikohozi kikavu,
  • Shida katika kupumua, 



na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha;
Homa ya mapafu (pneumonia),Kukosa pumzi, Kushindwa kufanya kazi kwa figo na hata kifo.

Jinsi ya Kujikinga.
  • Epuka mkusanyiko wa watu kadri inawezekana, na kama itakulazimu kuwa kwenyemkusanyiko jaribu kuwa katika umbali wa mita 1 au zaidi kati ya mtu na mtu,
  • Nawa mikono kwa sabuni (kwa sekunde 20 au zaidi)  mara kwa mara hasa unapokisha vitu au watu,
  • Epuka kugusa uso mara kwa mara,
  • Acha kuvuta sigara,
  • Tumia vifaa vya kujikinga unapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu kama vile maski na gloves.Haishauriwi kutumia vifaa hivi kama upo peke yako,
  • Kaa nyumbani na kujitenga unapohisi dalili hizo hapo juu. 
  • Nenda hospitali kama daili zinazidi.


Kinga na tiba;

Mpaka sasa hakuna kinga,chanjo wala tiba ya virusi vya korona. Juhudi zinafanywa na
mashirika mbalimbali ya afya duniani ili kupata tiba.
Kila nchi ina mfumo wake wa kupambana na Korona. 

Mambo ya kujua kuhusu virusi vya Korona;
  • Kutembea juani,sehemu yenye joto au baridi au kuoga maji ya moto hakuzuii maambukizi,
  • Maambukizi ya korona  yanapona kama magonjwa mengine,kuna uwezekano wa kupata maambukizi mapya baada ya kupona,
  • Kunywa pombe hakuzuii maambukizi,
  • Kuvuta sigara kunachangia maendeleo ya mgonjwa kuwa mabaya,
  • Mbu hawaambukizi korona,
  • Kufunika uso kwa kitambaa hakuzuii maambukizi,
  • Antibiyotik au dawa za malaria haziponyi korona ingawa kuna baadhi ya majaribio ya mchanganyiko wa dawa zinatomia dawa za malaria na virusi.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ualbino (Albinism)

 Ualbino ni nini? Ualbino ( albinism ) ni hali ya kiafya inayotokana na mwili kukosa uwezo wa kutoa homoni aina ya melanin . Homoni hii pamoja na kazi nyingine inahusika na utoaji wa rangi ya mwili. Ukosefu wa melanin huathiri ngozi, macho na nywele.  Ualbino ni hali ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ikumbukwe kuwa  Albino sio mgonjwa bali ni mlemavu wa macho, nywele na ngozi ambavyo huathiri maisha yake ya kila siku, hata kufupisha umri wa kuishi. Nje na binadamu ualbino unaathiri pia wanyama, samaki, wadudu, nyoka, mijusi, ndege na hata mimea (kwa mimea hutokana na ukosefu wa klorofili).  Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua kupendelea kuitwa "watu wenye ualbino" kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo au mizimu. Kuenea kwa Ualbino Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya 20,000 duniani ni albino, lakini kwa sababu zisizofahamika ba...

Ugonjwa wa Fistula ( Rectovaginal Fistula)

  Fistula ni nini? Fistula ni tundu lisilo la kawaida ambalo hutokana na kuungana kwa sehemu ya chini ya utumbo mpana (njia ya haja kubwa) na njia ya mkojo au njia ya uke, hivyo kumfanya mgonjwa kushindwa kuzuia haja au kutokwa na hajak ubwa ukeni.  Mara nyingi husababishwa na kujeruhiwa kwa sehemu hizo wakati wa kujifungua hasa kwa wanawake wanaozaa katika umri mdogo au wanaokosa msaada stahiki wakati wa kuzaa. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,  inakadiriwa kuwa wanawake zaidi ya milioni mbili kutoka Afrika na Asia wanaishi na ugonjwa huu, bila kupatiwa matibabu yoyote, kwa upande wa Tanzania wengi wamekua wakitafuta msaada kwa waganga wa jadi.   Nini Husababisha Fistula? Ugonjwa wa Fistula unaweza kusababishwa na mambo kadhaa ikiwemo yafuatayo; Majeraha wakati wa kujifungua, Maambukizi ya Mfumo wa uzazi (PID), Mgonjwa ya utumbo mpana kama vile Crohn , Saratani ya mfumo wa uzazi au utumbo mpana, Majeraha yanayotokana na ajali au upasuaji wa sehemu ya nyonga. Fi...

Saratani ya Matiti (Breast Cancer)

Utangulizi Saratani ya Matiti ni nini? Ni aina ya saratani inayoathiri matiti au maziwa kwa mwanamke au nadra pia kwa mwanaume. Hii hutokana na chembehai( cells) za sehemu yoyote ya ziwa au yote mawili kukua kuliko kawaida na kusababisha uvimbe, maumivu, kutokwa na majimaji,damu au usaha kwenye matiti. Wakati mwingine aina hii ya saratani inaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye kwapa, misuli ya kifua, mishipa ya damu, shingoni n.k.  Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2020, wanawake milioni 2.3 waligunduliwa kuwa na saratani ya matiti, takriban laki saba walifariki kwa saratani ya matiti. Kutoka mwaka 2015 hadi 2020 wanawake milioni 7.8 waligunduliwa kuwa na maradhi hayo, kuifanya saratani ya matiti kuwa ya kwanza kwa kuenea duniani. Ni muhimu kutambua kwamba sio kila uvimbe uliopo kwenye maziwa ni saratani, hivyo ni vyema kumuona Daktari unapokuwa na dalili yoyote nitakayotaja hapo chini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.  Nini husababisha sarata...