Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Msongo wa Mawazo (Depression)


Msongo wa mawazo ni nini?

Msongo wa mawazo  (Depression) ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo hutokana na pale mtu anaposhindwa kukabiliana na jambo linalomtatiza. Msongo wa mawazo huwapata watu wa rika na asili zote. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake  hupata msongo wa  mawazo zaidi kuliko wanaume. Msongo wa mawazo ni tatizo la kimwili pamoja na kiakili.

Dalili.
  • kujisikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa,
  • kukosa hamu ya kula au kula chakula kupitiliza,hasa vyakula vyenye madhara,
  • kukosa hamu ya tendo la ndoa,
  • kuwa na huzuni wakati wote na kujisikia mnyonge,
  • kusahau kirahisi au kupungua kwa uwezo wa kufikiria,
  • kujisikia mpweke au kukosa matumaini ya maisha,
  • kupungua kwa uwezo wa kimasomo kwa wanafunzi,
  • kuwa na hofu au kutokujiamini,
  • kupungua au kuongezeka uzito bila kupenda,
  • kushindwa kulala au kulala kupindukia,
  • kukosa utulivu wa nafsi,
  • kubadilika kwa siku za hedhi au kutokupata hedhi kabisa,
  • kubadilika kwa mwenendo ghafla k.v kugombana na ndugu, jamaa au marafiki bila sababu za msingi, kunywa pombe kupindukia au kutumia madawa ya kulevya,
  • kuwa na mawazo ya kujidhuru au kujiua.
Ili dalili hizi zihesabike kuwa ni msongo wa mawazo, kitaalamu ni lazima mtu azionyeshe kwa muda wa wiki mbili au zaidi. Kwa mfano, huzuni anayokuwa nayo mtu aliyefiwa huhesabika kama msongo wa mawazo kama itachukua wiki mbili au zaidi. Watoto wadogo wanaweza kuonyesha dalili tofauti na zile zilizotajwa hapo juu. 

Sababu.
Sababu za msongo wa mawazo  zimegawanyika katika makundi mawili ambazo ni kisaikolojia na kibayolojia. 

1.Sababu za kibayolojia.
  • Magonjwa sugu kama vile UKIMWI, figo, moyo, ini, TB, kisukari n.k,
  • Mtu kurithi vinasaba kutoka kwa mzazi/ wazazi.
2.Sababu za kisaikolojia.
  • Matukio yasiyofurahisha kama Ubakaji,Uvamizi, Ajali au Kufiwa, kutekwa nyara, 
  • Majanga kama Kimbunga, Mafuriko, Tetemeko la ardhi n.k,
  • Changamoto za kila siku za maisha kama vile Ugoni, Talaka, Mimba kuharibika, Kutoa mimba, Kutengana, Kufungwa, Kuuguza au Kukosa kazi, Ugomvi kwa wanandoa, Kusingiziwa jambo, Ushirikina n.k,
  • Matatizo sehemu za kazi Kufukuzwa kazi / Chuo, Migogoro kazini au Kustaafu kazi,
  • Mambo ambayo yanategemewa mtu kufurahi yanaweza kumsababishia msongo wa mawazo kama Kuoa au Kuolewa, Kuzaliwa mtoto, Kufaulu mtihani, Ajira mpya, kuhamia nyumba mpya, Kupata ujauzito nk. 

Namna ya kupunguza Msongo wa Mawazo
  • Tafuta chanzo cha msongo na epukana nacho,kabiliana nacho au kubaliana nacho, 
  •  Kuwa na mtazamo chanya kwamba hiyo ni changamoto inayokukabili na sio mwisho wa maisha, 
  •  Fanya mazoezi ili kupunguza mzigo wa hisia unaokuelemea na kuondoa msongo wa mawazo, 
  •  Epuka kuwa peke yako, washirikishe watu wa karibu matatizo yako na kuomba ushauri,
  • Pata muda wa kutosha wa kupumzika ikiwa ni pamoja na kulala, 
  • Epuka mazoea mabaya kama kunywa pombe au kutumia dawa kwa imani kwamba zitakupunguzia msongo wa mawazo, 
  • Jitahidi kula vizuri kwani mwili unategemea chakula ili uweze kufanya kazi vizuri, 
  •  Fanya vitu ambavyo vitakupa starehe kama kusoma vitabu, kusikiliza mziki, kwenda sehemu za burudani, na kuwa na mtu wa kukufariji. 
  •  Badilisha mazingira kwa kutembelea sehemu mbalimbali kama vile fukwe za bahari, mbuga za wanyama, bustani nk, 
  • Pata ushauri wa wataalamu (daktari, mwanasaikolojia nk), 
  •  Kutumia dawa kwa usahihi kila wakati na 
  •  Kuhudhuria kiliniki kila wakati kama ulivyopangiwa na wataalamu wa afya.
Hitimisho.
Msongo wa mawazo ni  ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine na ni janga kubwa ambalo jamii zetu hatulitilii maanani. Watu wengi wamepoteza ndugu na jamaa kwa sababu ya msongo wa mawazo lakini mara nyingi tatizo hili huunganishwa na matukio mengine. Elimu zaidi juu ya msongo wa mawazo inahitajika katika jamii uli kuongeza ufahamu na kukabiliana na ugonjwa huu.

Vyanzo.

Maoni

  1. Asante kwa Elimu keep the good work up

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Homa ya Findofindo (Tonsillitis)

Utangulizi   Findofindo ( Tonsillitis) ni nini?  Mafindofindo ni mashambulizi ya virusi au bakteria kwenye tezi za koo zijulikanazo kama findo. Asilimia 15 mpaka 30 ya mashambulizi haya yanatokana na bakteria ila asilimia kubwa hutokana na virusi.  Dalili za mafindofindo   Kwa kawaida ni ngumu kutofautisha kati ya maambukizi yatokanayo na bakteria na yale ya virusi ila leo nitakujuza siri ndogo. Zipo dalili za pamoja na zile za tofauti.  Zifuatazo ni dalili za pamoja za mafindofindo unazoweza kuzipata kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya bakteria na yale virusi  Maumivu ya koo Kupata shida katika kumeza  Homa kali ( Zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)  Maumivu ya kichwa  Maumivu ya sikio  Utando katika findo Dalili zifuatazo zinaasilimia kubwa sana kupatikana kwa mtu mwenye mashambulio yatokanayo na virusi.  Homa ( zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)   Uvimbe shingoni ( upande mmoja au pande mbili)   Maumivu ya kichwa  Kutokwa na kamasi  Kutokwa na machozi   Kumeza kwa shida  Maum

Shinikizo la damu (Hypertension)

Utangulizi Unaweza kuwa na shinikizo la damu (presha) kwa muda mrefu bila kuwa na dalili zozote. Muda wote huu ingawa unakuwa hauna dalili, uwepo wa shinikizo la damu huendelea kuathiri mishipa ya damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama vile magonjwa ya moyo na kiharusi.   Hivyo ni vizuri kujipima mara kwa mara ili kuepuka kuchelewa.     Shinikizo la damu hutokea taratibu kwa kadri umri unavyozidi kuongezeka, hivyo kuathiri karibu kila mtu anapofikia umri mkubwa. Upimaji wake ni rahisi kwa hiyo ni vema ukapima ili kuweza kupambana na ugonjwa huu kwa msaada wa daktari. Dalili Watu wengi wana shinikizo la damu bila kujua au kuwa na dalili. Ni wachahe wanaweza kuwa na dalili kama vile kuumwa kichwa,kutokwa na damu puani na kupata shida ya kupumua. Dalili hizi si maalumu ( spesific) na mara nyingi hazitokei mpaka shinikizo linapokuwa katika kiwango kinachohatarisha maisha. Shinikizo la damu hutokea kwa namna mbili; Kwanza:  Hutokea bila uwepo wa ugonjwa sab