Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Homa ya Findofindo (Tonsillitis)


Utangulizi 

Findofindo ( Tonsillitis) ni nini?

 Mafindofindo ni mashambulizi ya virusi au bakteria kwenye tezi za koo zijulikanazo kama findo. Asilimia 15 mpaka 30 ya mashambulizi haya yanatokana na bakteria ila asilimia kubwa hutokana na virusi. 



Dalili za mafindofindo 

Kwa kawaida ni ngumu kutofautisha kati ya maambukizi yatokanayo na bakteria na yale ya virusi ila leo nitakujuza siri ndogo. Zipo dalili za pamoja na zile za tofauti. 
Zifuatazo ni dalili za pamoja za mafindofindo unazoweza kuzipata kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya bakteria na yale virusi 
  • Maumivu ya koo
  • Kupata shida katika kumeza 
  • Homa kali ( Zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi) 
  • Maumivu ya kichwa
  •  Maumivu ya sikio 
  • Utando katika findo
Dalili zifuatazo zinaasilimia kubwa sana kupatikana kwa mtu mwenye mashambulio yatokanayo na virusi.
  •  Homa ( zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi) 
  •  Uvimbe shingoni ( upande mmoja au pande mbili) 
  •  Maumivu ya kichwa 
  • Kutokwa na kamasi 
  • Kutokwa na machozi 
  •  Kumeza kwa shida 
  • Maumivu ya koo 
  • Utando mweupe koni 
  •  Kikohozi 
  •  Kupiga chafya

Je ni nini cha kufanya pindi unapokuwa na  dalili hizi? 

Pindi uonapo dalili hizi ni vizuri kufika kituo cha afya kwani kama maambukizi haya yanatokana na bakteria basi utalazimika kutumia dawa malum kwa ajili ya kuua bakteria ( Antibiotics) lakini kama maambukizi yanatokana na virusi basi hutohitajika kutumia dawa hizo na badala yake utashauriwa kutumia dawa za maumivu na kunywa maji mengi kwa siku. 

Ujumbe muhimu

Tambua tofauti za mashambulizi ya virusi na yale ya bakteria ili ukwepe kutumia antibiotics bila sababu.



                                                

                                                    Imetayarishwa na Dr. Umari Ali Jokho,MD.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Msongo wa Mawazo (Depression)

Msongo wa mawazo ni nini? Msongo wa mawazo  ( Depression ) ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo hutokana na pale mtu anaposhindwa kukabiliana na jambo linalomtatiza. Msongo wa mawazo huwapata watu wa rika na asili zote. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake  hupata msongo wa  mawazo zaidi kuliko wanaume. Msongo wa mawazo ni tatizo la kimwili pamoja na kiakili. Dalili. kujisikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa, kukosa hamu ya kula au kula chakula kupitiliza,hasa vyakula vyenye madhara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuwa na huzuni wakati wote na kujisikia mnyonge, kusahau kirahisi au kupungua kwa uwezo wa kufikiria, kujisikia mpweke au kukosa matumaini ya maisha, kupungua kwa uwezo wa kimasomo kwa wanafunzi, kuwa na hofu au kutokujiamini, kupungua au kuongezeka uzito bila kupenda, kushindwa kulala au kulala kupindukia, kukosa utulivu wa nafsi, kuba

Shinikizo la damu (Hypertension)

Utangulizi Unaweza kuwa na shinikizo la damu (presha) kwa muda mrefu bila kuwa na dalili zozote. Muda wote huu ingawa unakuwa hauna dalili, uwepo wa shinikizo la damu huendelea kuathiri mishipa ya damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama vile magonjwa ya moyo na kiharusi.   Hivyo ni vizuri kujipima mara kwa mara ili kuepuka kuchelewa.     Shinikizo la damu hutokea taratibu kwa kadri umri unavyozidi kuongezeka, hivyo kuathiri karibu kila mtu anapofikia umri mkubwa. Upimaji wake ni rahisi kwa hiyo ni vema ukapima ili kuweza kupambana na ugonjwa huu kwa msaada wa daktari. Dalili Watu wengi wana shinikizo la damu bila kujua au kuwa na dalili. Ni wachahe wanaweza kuwa na dalili kama vile kuumwa kichwa,kutokwa na damu puani na kupata shida ya kupumua. Dalili hizi si maalumu ( spesific) na mara nyingi hazitokei mpaka shinikizo linapokuwa katika kiwango kinachohatarisha maisha. Shinikizo la damu hutokea kwa namna mbili; Kwanza:  Hutokea bila uwepo wa ugonjwa sab